Wakimbizi wote wenye asili ya Kisomali nchini Kenya, wameamriwa kuondoka katika maeneo ya mijini na kurudi kambini baada kuwepo kwa milipuko ya mara kwa mara.
Misaada haitatolewa tena kwa yeyote ambaye atakuwa mjini, amesema mkuu wa shirika la wakimbizi la umoja wa mataifa.

Misaada haitatolewa tena kwa yeyote ambaye atakuwa mjini, amesema mkuu wa shirika la wakimbizi la umoja wa mataifa.
Milipuko hiyo imekuwa ikitokea mara kwa mara katika maeneo yenye idadi kubwa ya watu wenye asili ya Kisomali, kama vile mkoa wa Kaskazini Mashariki na mtaa wa Eastleigh iliyoko mjini Nairobi.
Mashambulizi hayo yanaaminika kufanywa na watu wanaoaminika kuwa wanachama cha kundi la Kiislamu la Al Shabab.