Rais Jacob Zuma amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa kiongozi wa
chama tawala nchini humo cha African National Congress ANC.
Zuma alipata idadi kubwa ya kura zilizopigwa na wajumbe elfu nne wa chama
hicho wakati wa mkutano wao uliofanyika Mangaung.
Tangu mwanza wa zoezi hilo, Rais Zuma, alitarajiwa kushinda na idadi kubwa ya
kura dhidi ya mpinzani wake wa pekee ambaye pia ni naibu makamu wa rais Kgalema
Motlanthe.
Bwana Motlanthe sasa amepoteza nafasi yake ya naibu kiongozi wa chama hicho
na mahala pake pamechukuliwa na mfanyabiashara maarufu na mwanaharakati dhidi ya
ubaguzi wa rangi Cyril Ramaphosa, ambaye sasa atakuwa makamu wa rais wa Afrika
Kusini.
Ramaphosa makamu mpya wa rais
Mshindi wa nafasi hiyo ndiye atakayekuwa na nafasi ya kushinda uchaguzi wa
mwaka 2014.
Chama cha ANC kimeshika hatamu nchini Africa Kusini tangu kumalizika kwa
utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994.
Polisi nchini humo, hapo jana waliwatia mbaroni watu wanne baada ya taarifa
kuzagaa kwamba walikuwa na mpango wa kulipuwa ukumbi unaotumiwa na wajumbe hao
wa chama cha ANC.
Baada ya uchaguzi huo kucheleweshwa kwa masaa kadhaa, zoezi la kupiga kura
lilianza saa sita usiku na kukamilika majira ya saa moja asubuhi kwa saa za
Afrika Kusini.
Wajumbe hao walioonekana wamechoka huku wakijifunika mablanketi walionyesha
vidole vyao vikiwa na alama ya wino.
Wajumbe hao wamekuwa wakipiga kura kwa ajili ya nafasi ya uongozi wa juu wa
chama hicho.
Wafuasi wa rais Zuma, tayari wanaendelea kusheherekea, kufuatia ushindi huo
mkubwa.
Rais Zuma analaumiwa kwa kushindwa kupunguza umaskini au kutatua tatizo la
ufisadi ndani ya chama cha ANC na serikali, wakati mwezi wa nane mwaka huu watu
walishangazwa na jinsi polisi walivyowapiga risasi na kuwauwa wachimba madini 34
ambao walikuwa wamegoma |
0 Comments