Na Maganga One Blogger.

Happy New Year Wapenzi na Mashabiki wa Maganga One Blog...Kwa furaha tele na Afya bora niliyojaaliwa na Mwenyezi  Mungu muumba wa ardhi na mbingu kwa kuuona vyema mwaka 2013.Neno bora kwangu ni Alhamdulillah nimeuona mwaka salama mimi na familia yangu.Ilikuwa jana tu ila naruhusiwa kusema mwaka jana 2012 kwa upande wangu ulikuwa mwaka mzuri sana kwa mengi.Nimejifunza mengi sana mapya,nimepata changamoto nyingi sana na ndani ya changamoto hizo ndipo nikajua upeo wa akili yangu,maarifa yangu na uwezo wa nguvu zangu nilizojaaliwa na Mwenyezi Mungu.

Ukiwa na akili na ukaweza kuzitumia watu watakuona una akili,ukiwa na maarifa na ukaweza kuyatumia watu watakuona una maarifa na ukiwa na nguvu kadhalika ukaweza kuzitumia jua watu wataona kama una nguvu.
Swali linakuja je vitu hivi unavitumia kwa maslahi ya jamii au unavitumia kwa manufaa yako binafsi?
Jibu linakuja kwamba navitumia kotekote,yani kwa maslahi ya jamii na huku nikivitumia kwa manufaa yangu binafsi.

Ndugu zangu,ulimwengu tulionao sasa sio tena wa kutumainia akili za mwenzako,maarifa ya mwenzako na nguvu za mwenzako.Ukiwa kama mwanaadamu uliye na viungo timilifu na akili timamu jaribu kutumia kile ulichojaaliwa ili kunufaisha umma huku ukijinufaisha na mwenyewe.
Kwa kila mwenye kusoma haya maelezo nina imani kabisa ana akili timilifu za kuelewa nini ninamaanisha juu ya hili.
Umejaaliwa nguvu tafadhali zitumie nguvu zako kwa maendeleo ya wote na ya kwako pia,umejaaliwa akili tafadhali zitumie akili zako kwa maendeleo ya jamii yako na familia yako..kadhalika umejaaliwa maarifa usisite kuyaweka bayana maarifa yako ili kuwasaidia wenzako.
Haitakuwa jambo la busara kulalama kila kukicha kwa kuwapa lawama wenzako hali yakuwa na wewe una akili zako,nguvu zako na maaraifa yako.

Pichani juu ni mimi Maganga One,ukiiangalia picha hiyo ninakuonyesha ishara ya kupiga saluti..saluti hiyo najipigia mwenyewe na kwa upande wa pili nakupigia na wewe msomaji,sikuwa mchoyo wa saluti yangu kwani nimeitumia kotekote..Je saluti hiyo unaijua maana yake?
Tukirudi kwenye T~shirt niliyovaa ina wanajeshi wenye zana za kivita na chini nimevalia suruali ya kijeshi.Ukiniita mwanajeshi sitabisha kwani ndani ya nafsi yangu najijua mimi ni mwanajeshi.Kwa kuwa mimi sio mchoyo wa akili na maarifa niliyojaaliwa ninapenda kuchangia na wewe kile nilichojaaliwa,ila je upo tayari kuigawa saluti yako kwa wengine kama nilivyofanya mimi? je upo tayari kutumia akili yako kwa maslahi ya wengine?

Waungwana nimefumbafumba maandishi yangu kuona kama unaweza kutumia akili yako na maarifa yako katika mwaka 2013.kama utakuwa tayari kuitumia akili yako kwa manufaa ya wengi Mungu akubariki na kama utakuwa tayari kuyatumia maarifa yako kwa manufaa ya wengi Mungu akubariki.
Ila ukishindwa kutumia akili yako kwa kutegemea ya mwenzako usije ukamlaumu mtu.
Nawatakia kila la heri kwa mwaka 2013
Tutumie akili na maarifa katika kujikwamua kimaisha.
Tuheshimu vyombo vya dolaTuheshimu serikali yetu
Tuheshimu Viongozi wetu.
Asanteni sana.
Maganga One.

Tumia akili yako kujua What i`m talking about..!!