Bwana harusi ndugu yetu Mr Mansour Omar jana aliutangazia umma  kwamba na yeye amejiunga rasmi katika chama cha waliooa duniani.Pichani bi harusi Mrs Mansour akijiandaa kukata keki na kumlisha mumewe.
 Akiwa mwenye tabasamu bwana harusi aligeuza shingo kupokea salamu za pongezi kwa rafiki na ndugu zake wa karibu hapo jana.
Ebwana vipi kila kitu poaa? Aisee poa kabisaaa....Bwana harusi anaonekana akimuuliza mpambe wake .Maharusi na harusi nzima ilikwenda salama na ilipendeza kwa ujumla,kila mmoja alifurahia harusi hii hapo jana.
Kama kawaida kila mmoja aliyefika ukumbini alipenda kupata picha ya pamoja na maharusi iwe kama kumbukumbu bora maishani.Pichani baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki wa karibu wa maharusi wetu hapo jana wakipata picha.
Penye watoto ujue pana Amani na watoto ni baraka,kwa picha hii inaonyesha maharusi watakuwa na Amani na ndoa yao iwe na baraka maishani mwao insh'Allah.Maganga One Blog inawatakia maisha mema na yenye heri ndani yake.Kwa picha zaidi za harusi hii ni hapo baadae.