Habari za jumapili watu wangu..!!Kama kawaida yetu kila jumapili nikipata fulsa huwa napenda kutumia muda wangu wa spare kujumuika nanyi kwenye ukurasa kuwaletea fikra zangu.Leo nimekuja na ujumbe mwingine kabisa ili kujaribu kuielemisha jamii.Binaadamu wachache sana wenye tabia ya kumsifia mwenzake kwa matamshi au hata kwa vitendo,sio kweli kwamba utamani na wewe kusifiwa ila bado hujapata sifa za kusifiwa...jitahidi kuna nafasi nyingi za kusifiwa pindi ukifanya sifa ya kusifiwa.

Imekuwa kawaida yangu kumpa sifa kila ninayemuona anastahili sifa zangu,Tofauti na vijana wengi ninaobahatika kuwaona au kuwasikia kwamba mara nyingi ukaa na kuanza kuwaponda wenzao hali wao hawana hata moja lifaalo.Hii sio tabia nzuri na wala sio sifa ukasema watu watakusifu,badala yake watakukashifu kwa kile unachokifanya.Unakuta kijana anajituma katika kutafuta maisha kwa njia moja au nyingine ,badala ya kumsifu na kumpa moyo wa kujituma zaidi,vijana wenzake ukaa chini na kuanza kumponda kwa maneno ya kejeli n.k.

Pichani ni binti yangu,Binti yangu alikuwa akimpigia makofi na kumpongeza kila mkimbiaji aliyepita mbele ya macho yake katika kumpa moyo wa jitihada anazoonyesha mkimbiaji huyo.Sio kwamba binti yangu aliwafahamu wakimbiaji wale laah...Ila ilimpasa kumpa pongezi kila mkimbiaji kwa jitihada zake kwani aliona anastahili kufanya vile.Hii ni sifa moja wapo ambayo nampongeza binti yangu kwa kile anachokifanya angali mtoto,na nawaomba ndugu zangu wasomaji tuwe na taratibu za kuwasifu wenye kustahili kusifiwa kwani ikifika zamu yako nawe utasifiwa kama ulikuwa ni msifiaji mzuri.Ila usitegemee kusifiwa hali ya kuwa wewe ni mkuu wa kuponda na majungu...sifa zako zitakuwa mbaya kwa kuwa na wewe ulikuwa mbaya kwa wenzako.

Jumapili ya leo nitaishia hapaa,kwa kusema jiwekee utaratibu wa kumpa sifa kila unayeona anastahili sifa hata kama humpendi,hautapata dhambi kwa kumsifia mwenzako ila utajijengea dhambi kwa kumkashifu mwenzako.Jumapili njema.
                                                                Maganga One - Blogger.
                                                                magangaone@gmail.com
                                                                +32 049 222 33 25