Wachezaji wa Ivory Coast wakishangilia bao lao.
Ivory Coast imeanza kampeini yake ya kuwania kombe la mataifa ya
Afrika kwa kuilaza Togo kwa magoli mawili kwa moja katika mechi yao ya
ufunguzi ya Kundi D.
Ivory
Coast ilipata bao lake la kwanza kunako dakika ya nane kupitia kwa
mchezaji Yaya Toure na kwa mara nyingine, wachezaji hao wa Ivory Coast
wanatafuta fursa ya kutwaa kombe hilo ambalo liliwaponyoka mwaka
uliopita.
Nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba, analiongoza tena timu hiyo, kwa fainali hizo ambazo ndizo za mwisho atakazoshiriki.
Licha ya wengi kuipa timu hiyo ya Ivory Coast
nafasi kubwa ya kushinda mashindano ya mwaka huu, The Elephants
hawakucheza mechi ya kusisimua katika kipindi cha kwanza.
Mara ya Mwisho Ivory Coast, ilishinda kombe hilo ni mwaka wa 1992.
Togo nayo inaongozwa na mshambulizi wa Tottenham, Emmanuel Adebayor.
Dakika ya 44, Yahya Toure, nusura afunge bao la pili, lakini mkwaju wake uligonga mlingoti.
Ushirikiano kati ya Didier Drogba, Yahya Toure and Gervinho umeonekana kuwa nguzo ya timu hiyo ya Ivory Coast.
Dakika moja baadaye Togo ikasawazisha baada ya walinda lango wa Ivory Coast kufanya masihara, kwenye eneo la hatari.
Kufikia wakati wa mapumziko timu hizo mbili zilikuwa zikitoshana na nguvu ya kufungana bao moja kwa moja.
Lakini katika kipindi cha pili, Ivory Coast
iliimarisha mashambulizi yake na kunako dakika ya 87, ivory coast
ikapata bao lake la pili kupitia kwa mchezaji Gervinho.
Ivory Coast sasa inaongoza kundi hilo la alama tatu huku Togo ikiwa bila alama yoyote.
Kinyume na ilivyotarajiwa, mechi hiyo iligeuka
na kuwa maonyesho ya nguvu, baina ya wachezaji kadhaa wanaoshiriki
katika ligi mbali mbali za kulipwa na mara nyingi ilikuwa kati ya Kolo
Toure na Adebayor na Vincent Bossou na Didier Drogba ambao walifanya
makosa mengi na hivyo kuhujumu mtiririko wa mechi hiyo.
Mechi ya pili ya kundi hilo kati ya Tunisia na Algeria itaanza mwendo wa saa tatu za usiku majira ya Afrika Mashariki.
|
0 Comments