Na Issa Mnally BAADHI ya akinadada wanaofanya
biashara haramu ya kujiuza katika maeneo ya Jiji la Dar, wameeleza kuwa
licha ya kupewa kashikashi na jeshi la polisi na wakati mwingine
kukamatwa na kupelekwa mahakamani, hawawezi kuiacha ‘kazi’ hiyo kutokana
na ugumu wa maisha.Wadada hao waliyasema hayo, juzi Jumatano baada ya kunaswa na paparazi
wetu maeneo ya Sinza Afrikasana pembeni ya Corner Bar ikiwa ni siku
chache baada ya baadhi yao kukamatwa na polisi ambapo walisema biashara
hiyo ndiyo maisha yao. Walisema, hawapendi kuifanya lakini wanalazimika kutokana na maisha duni waliyonayo.Nani asiyependa kulala usiku na familia yake? Ukituona barabarani ujue
hali ni mbaya. Hata kama polisi wanatukamata lakini wanatuachia na
tunarudi sokoni kama kawaida,” alisema changu mmoja aliyejitambulisha
kwa jina la Zuena na kuongeza: “Wateja wetu wenyewe wanajua kuwa hii
nguvu ya polisi ni ya soda tu, wakiona tumepigwa ambushi kidogo
wanasubiri zipite siku chache kisha tunaendeleza harakati zetu, sisi
bila kuja kujiuza hatuwezi kuwasomesha watoto wetu wala kuwalisha.”Katika hali ya kushangaza wakati changudoa huyo akizungumza hayo, wapo
waliokuwa wakimshawishi paparazi wetu anunue ngono kwa maelezo kuwa,
hali ni mbaya kwani polisi wamekuwa wakifanya doria mara kwa mara.
“Sasa, achana na mambo ya kutuhoji bwana, tutoe basi kama vipi tukuuzie
mambo kwa bei ya ofa. Cheki nilivyojaaliwa,” alisema binti mmoja ambaye
ukikutana naye mchana unaweza kusema, ‘mke si ndiyo huyu’.Hata hivyo, katika pitapita ya mwandishi wetu maeneo mengi kama vile
Kinondoni, Sinza Mapambano, Mwenge Bamaga na Buguruni, madadapoa hao
wameonekana wakiendelea kujiuza kwa kuibia huku wakiwa makini na kila
mteja anayewatokea.Aidha, gazeti hili linalipongeza Jeshi la Polisi jijini Dar kwa
operesheni ambazo limekuwa likizifanya kwani kwa namna moja ama nyingine
kasi ya biashara hiyo imepungua licha ya kwamba wanatakiwa kuongeza
nguvu zaidi. Pia taasisi za ustawi wa jamii na serikali kwa jumla
zinatakiwa kuangalia mbinu mbadala za kuweza kuwaondoa akinadada hao
kwenye mazingira hayo hatarishi. |
0 Comments