Flaviana Matata, mwanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania. |
FLAVIANA Matata, mwanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania,
ameshinda tuzo ya ‘Nigeria’s Next Super model 2012’ inayomtambulisha
kama Mwanamitindo Bora mwenye Mvuto Afrika (Africa’s Most Outstanding
Model 2012).
Ushindi wa tuzo hiyo ya pekee kwa aina yake,
umefungua milango ya kutambulika zaidi Matata hata kulivusha kimataifa
jina la Tanzania katika tasnia ya mitindo na mavazi.
Akiongelea ushindi wa tuzo hiyo, Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Compass Communication Tanzania Limited, Maria
Sarungi Tsehai alisema ushindi wa Matata ni mafanikio mengine ya
kujivunia. Tsehai ndiye aliyevumbua kipaji cha Matata.
Kwa mara ya kwanza Flaviana aliibuka kwenye mashindano ya Miss
Universe akiweka rekodi ya mrembo wa kwanza kushinda taji hilo nchini.
Aliiwakilisha nchi kwenye mashindano ya ‘World Miss Universe’ mwaka 2007 na kumaliza nafasi ya sita, mjini Mexico City, Mexico.
Matata pia ni balozi wa taasisi ya kusaidia watoto
(SOS) na Matata Diamond Empowerment Fund (Def) ya Marekani, ambapo
anafanya kazi sambamba na mwanamitindo na msanii wa vipindi vya
televisheni Kim Kardashian.
Kimwana huyo pia ana mkataba na kampuni ya mitindo
ya Afrika Kusini inayojulikana kama Boss Models SA, ambapo awali pia
aliwahi kufanya kazi na Kampuni ya Models pia ya Afrika Kusini.
Kwa sasa makazi yake yako mjini New York, Marekani ambapo pia anafanya kazi za mitindo katika Miji ya London, Paris na Milan.
Kwa sasa makazi yake yako mjini New York, Marekani ambapo pia anafanya kazi za mitindo katika Miji ya London, Paris na Milan.
Tuzo hiyo imeboresha zaidi fursa yake kutambulika kimataifa tangu alipoibuka mara ya kwanza nchini kupitia mashindano ya urembo.
Miongoni mwa mafanikio aliyopata kupitia sanaa ya
mitindo ni umiliki wa taasisi binafsi ya Flaviana Matata Foundation,
ambapo amekuwa akisomesha watoto wa kike kila mwaka.
Aidha, aliwahi kushinda tuzo ya mwanamitindo bora ya jarida la kila wiki Nigeria ‘Arise Magazine Fashion’ mjini Lagos mwaka juzi.
Aidha, aliwahi kushinda tuzo ya mwanamitindo bora ya jarida la kila wiki Nigeria ‘Arise Magazine Fashion’ mjini Lagos mwaka juzi.
Pia aliwahi kuingia kwenye orodha ya wanamitindo bora 10 wenye asili ya Afrika waliotangazwa na jarida la Essence Magazine.
Isitoshe, umaarufu wake ulimpa nafasi ya
kushirikiana na wanamitindo mbalimbali wa kimataifa na miongoni mwao ni
Tommy Hilfiger, Jason Wu, Alexander McQueen na SUNO.
Wengine katika orodha hiyo ni Catherine Malandrino, Ally Rehmtullah, Rachel Roy, Charlotte Ronson, Tony Burch na Vivienne Westwood.
Wengine katika orodha hiyo ni Catherine Malandrino, Ally Rehmtullah, Rachel Roy, Charlotte Ronson, Tony Burch na Vivienne Westwood.
Majarida mbalimbali ya kimataifa yametumia picha zake kadhaa na hii ni kwa sababu ya mafanikio yake kwenye sanaa ya mitindo.
0 Comments