Kuna taarifa za kutatanisha kuhusu operesheni iliyofanywa na Ufaransa
ili kumkomboa mateka mmoja anayezuwiliwa na wapiganaji wa al-Shabaab
nchini Somalia.Msemaji wa kundi hilo la wapiganaji alieleza kuwa operesheni hiyo
iliyofanywa Ijumaa usiku na makamando haikufanikiwa, na kwamba Mfaransa
mmoja amekufa.
Serikali ya Ufaransa haikusema kitu kuhusu
operesheni yao hiyo ya jana usiku ambayo inaonesha ilifanywa na
makamando ambao walipelekwa kusini mwa Somalia kwa helikopta.
Msemaji wa al-Shabaab amearifu kuwa operesheni hiyo ilishindwa na kuna taarifa kuwa mzungu mmoja amekufa kwenye tukio hilo.
Tovuti moja mashuhuri ya habari nchini Ufaransa
inaarifu kuwa habusu mwenyewe, askari wa ujasusi wa Ufaransa aliyetekwa
mwaka wa 2009 ameuwawa, lakini taarifa hizo hazikuthibitishwa.
Inavoelekea operesheni hiyo inahusiana na
Ufaransa kuamua kuingilia kati kijeshi nchini Mali - uamuzi ambao
serikali inatambua kuwa utaathiri piya hali ya mateka 9 wa Ufaransa
wanaozuwiliwa sehemu mbali-mbali za Afrika. |
0 Comments