Watu wawili, wameuawa katika makabiliano kati ya waandamanaji, na plisi mjini Cairo.
Kwa mujibu wa maafisa wa afya, wawili hao walipigwa risasi wakiwa kando ya medani ya Tahrir.

Makabiliano kati ya waandamanaji na polisi.
Ripoti zinasema kuwa 
 mwanamume mmoja alifariki katika eneo la Tahrir wakati wa pili alifariki hospitalini.
Zaidi ya watu 50 wamefariki katika makabilino katika baadhi ya miji nchini misri katika wiki moja iliyopita.
Hizi ghasia zimesemekana kuwa mbaya zaidi tangu rais Morsi kungia mamlakani.
Wakosoaji wanamtuhumu kwa kuhujumu faida za mapinduzi ra kiraia.
Rais Mursi ameenda mjini Berlin Ujerumani kuomba mkopo unaohitajika sana licha ya ghasia, zinazoendelea kwa sikub ya saba mjini Cairo.
Serikali ya Morsi iko kwenye mazungumzo na shirika la fedha duniani kuhusu mkopo wa dola bilioni 4 nukta nane lakini makubaliano ya mwanzo kuhusu mkopo huu yalijikokota kwa sababu ya hofu kuwa mgogoro wa kisiasa unaoshuhudiwa Misri kwa sasa huenda ukahujumu mageuzi ya kifedha.
Bwana Morsi atajaribu kumshawishi chansela wa ujerumani, Angela Merkel kuwa serikali yake ingali inasisitiza kuwa demokrasia sharti, itazingatiwa.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa hii ni ishara ya maswala ya kifedha ya nje yalivyo ni muhimu kwa Misri na ndiposa rais Morsi akaamua kufanya safarai nje wakati nchi inatokota.