Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai.
MWANDISHI wa Habari wa Kituo cha Redio Kwizera wilayani Kakonko,
Mkoa wa Kigoma, Issa Ngumba (45), ameuawa kwa kupigwa risasi na
kunyongwa na watu wasiofahamika.
Habari zilizopatikana jana zimeeleza kuwa mwili wa
mwandishi huyo ulikutwa porini, siku tatu tangu alipotoweka nyumbani
kwake katika mazingira ya kutatanisha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai
alithibitisha tukio hilo, lakini akasema asingeweza kulizungumzia kwa
undani kwa kuwa polisi walikuwa bado eneo la tukio.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema
mwandishi huyo alikutwa jana akiwa amekufa, huku mwili wake ukiwa na
majeraha ya risasi na ukiwa umenyongwa na pembeni yake kulikuwa bastola iliyokuwa imetelekezwa pamoja na simu zake mbili za mkononi.
“Mwili wake ulipatikana jana katika Pori la Mlima
Kajuluheta ulioko katika Kijiji cha Muhange, Kakonko asubuhi baada ya
wananchi kufanya msako wa siku tatu tangu Jumapili iliyopita ikiwa ni
siku moja baada ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha,” alisema
mmoja wa mashuhuda hao.
Imeelezwa kuwa pamoja na vifaa hivyo, pia katika
eneo hilo la tukio kulikutwa risasi tano na katika mfuko mmoja wa
suruali ya marehemu, kulikuwa na noti moja ya Sh10,000.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Kigoma
(KPC) Deogratius Nsokolo alisema: “Sisi ndiyo kwanza tunaelekea eneo la
tukio, lakini waandishi wa Wilaya ya Kibondo ambao waliwahi kufika eneo
la tukio na kushuhudia uchunguzi wa daktari, wameeleza kuwa marehemu
amekufa kwa kunyongwa na kupigwa risasi mkono wa kushoto.”
“Tunaelekea Wilaya ya Kakonko kutoka Kigoma Mjini,
lakini daktari amesema maiti inaonekana kunyongwa shingo na kupigwa
risasi mkononi.”
Alisema mwili huo ulifanyiwa uchunguzi na daktari Primus Ijumaa wa Hospitali ya Wilaya ya Kibondo.
Kamanda Kashai alisema jeshi lake linasubiri
taarifa ya daktari aliyefanya uchunguzi wa mwili wa marehemu pamoja na
taarifa za awali za uchunguzi kabla ya kutoa taarifa kamili kwa
waandishi wa habari.
Naibu Mhariri wa Kituo cha Redio Kwizera
kinachorusha matangazo yake kutoka wilayani Ngara mkoani Kagera, Seifu
Upupu alisema mwandishi huyo alipotea tangu Januari 5, mwaka huu saa
kumi na moja jioni.
“Simu zake zilikuwa zikiita bila kupokewa kwa muda
wote na hadi jana (juzi) zikawa hazipatikani kabisa,’ alisema Upupu na
kuongeza:
|
0 Comments