Serikali ya Afrika Kusini inasema rais wa zamani wa nchi hiyo, Nelson Mandela, hajambo baada ya ugonjwa wa mapafu na upasuaji wa kutoa mawe kwenye kibofu nyongo.Alikuwa hospitali kwa majuma kadha mwezi wa Disemba.
Taarifa rasmi iliwanukuu madaktari waliomtibu wakisema kuwa Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94, amepata nafuu na afya yake inazidi kutengenea.
Rais huyo amebaki nyumbani kwake mjini Johannesburg tangu alipotoka hospitali siku 11 zilizopita.