Rais wa Ghana akiapishwa.
Chama kikuu cha upinzani nchini Ghana, kimesusia
sherehe za kuapishwa kwa rais John Mahama kufuatia uchaguzi wa mwezi
uliopita uliokumba na utata.
Chama cha New Patriotic Party (NPP) kimedai Bwana Mahama alishinda uchaguzi huo kwa njia ya udanganyifu.
Matokeo
rasmi yalimpa Bwana mahama ushindi wa asilimia 50.7, ya kura zaote
zilizopigwa, kiwango ambacho kinamfanya kueouka duru ya pili ya uchaguzi
dhidi ya mgombea wa chama cha NPP Nana Akufo-Addo, ambaye alipata
47.7%.
Kabla ya kuapishwa kwake rais Mahama alitoa wito
kwa rais wa nchi hiyo kuwa watulivu na kuwa na umoja, ili kudumisha
demokrasia yao ambayo kwa sasa inakisiwa ndiyo thabiti zaidi barani
Afrika.
Bwana Mahama alikuwa makamu wa rais hadi kifo cha ghafla cha rais John Atta Mills mwezi Julai mwaka uliopita. |
0 Comments