Alidai kuwa yeye alikuwa akivuka kwenda upande wa
pili lakini akiwa katikati ya barabara, walitokea vijana waliovalia
nguo za kirai na kumweleza yeye pamoja na hao wasichana kuwa wako chini
ya ulinzi.
Alidai kuwa baada ya kuwaweka chini ya ulinzi waliwaambia kuwa
kwa wakati huo walikuwa wanaendesha doria kwa ajili ya kukamata
makahaba na watu wanaoshirikiana nao.
“Mheshimwa askari hao,
walinihusisha mimi kama mteja wa makahaba na baada ya muda yalitokea
magari mawili ambayo moja lilikuwa na askari wanne wenye silaha na
lingine likiwa na mtu mmoja ambaye kwa sasa ni RCO mkoani Arusha,
Camillius Wambura na dereva,” alidai
.
Alidai kwamba alimfahamu Wambura kwa sababu
aliwahi kuwa na kesi katika Mahakama ya Kisutu, wakati huo na alikuwa
akishikilia jalada lake.
Alendelea kudai kuwa baada ya Wambura kumwona, alimhoji kulikoni kuwepo uraiani wakati kwa mawazo yake aliamini yupo jela.
“Nilimjibu
mahakama iliniachia baada ya kuniona sina hatia. Hakuniamini akatoa
pingu nikafungwa na kupandishwa kwenye gari lililokuwa limebeba askari
wanne na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay Desemba,”
alidai Rwanda.
Mshtakiwa huyo alidai kuwa alipofika katika kituo
hicho cha polisi, baadaye walimhamishia katika kituo kingine cha polisi
cha Kijitonyama ambapo walianza kumtesa. Alidai kuwa kuanzia Desemba 11
hadi 19,2010 askari walikuwa wakibadilishana kwa ajili ya kumtesa na
kwamba walikuwa wakimvua nguona kumwagia maji na kumpiga.
Aliendelea kudai kuwa Desemba 20, mwaka 2010
nyakati za usiku alifika askari wa nyota moja akiongozana na askari
wengine wakamchukua hadi mapokezi ambako askari walimwambia kuwa hana
thamani wala faida yoyote kwa sababu alimjibu bosi wao jeuri na kwamba
watamnywesha simenti.
Baadaye yule askari wa nyota moja alitoa jalada
moja kubwa na kuniambia nisaini, ilinilazimu kukubaliana naye kulingana
na mateso na kipigo nilichokipata.
Hakimu Tarimo aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 7, mwaka huu kwa ajili yamshtakiw ahuyo kuhojiwa na upande wa mashtaka.
Katika kesi hiyo namba 256 ya 2010, Rwanda na wenzake Samwel Hezron, Hati Jawadu na Ismail Juma.
0 Comments