Salum Mohamed ‘Sam wa Ukweli’.Kwa mujibu wa chanzo makini, Sam alifanya makubaliano na wasaidizi wa rais wakamtaka kuwa miongoni mwa wasanii ambao wangetumbuiza kwenye sherehe ya Mwaka Mpya iliyofanyika Msoga, Pwani (nyumbani kwa rais) lakini jamaa akaingia mitini.
 Baada ya kuzinyaka habari hizo, Centre Spread ilimtafuta Sam na alipopatikana alikiri kuwa ni kweli alitakiwa kufanya shoo hiyo, akafafanua:
“Kikwete ni mjomba wangu kabisa na ni kweli kwamba nilialikwa kwenda kufanya shoo Msoga siku ya Mwaka Mpya, nikaenda kuanza kufanya maandalizi ikiwa ni pamoja na kusaidia kupamba pale nyumbani, kazi ambayo nilishirikiana na mtoto wa rais, Miraji.
“Kwa bahati mbaya, siku ilipofika mwanangu aliungua na maji ya moto wakati akicheza na wenzake, ikanibidi nimpeleke hospitali ndiyo maana nikashindwa kwenda kwenye shughuli hiyo,” alisema Sam.