Serikali ya rais Morsi inakabiliwa na upinzani mkali

Kundi kubwa zaidi la upinzani nchini Misri limesema halitahudhuria mazungumzo yanayoandaliwa na Rais Mohamed Morsi hadi pale masharti yatakapotimizwa.
Mkutano huo ulinuia kumaliza machafuko ambayo yamekuwa yakiendelea katika miji kadhaa katika siku za hivi karibuni.
Awali Rais Morsey alitangaza hali ya hatari ya muda wa mwezi mzima katika miji ya Port Said, Suez na Ismailiya kufuatia siku kadhaa ya maandamano na fujo.
Amesema kuwa pia ameweka amri ya kutotoka nje usiku kucha. Kiongozi wa kundi la upinzani la Free Egyptians Party, Dr Ahmed Saeed, ameaimbia BBC kuwa rais Mosri anapaswa kufanya juhudi zaidi kurejesha imani ya wananchi.

Mapema leo Rais wa Misri Mohammed Morsi ametangaza hali ya tahadhari katika miji ya Port Said, Suez na Ismalia baada ya siku kadhaa za machafuko makali.
Kuanzia Jumatatu na kwa siku 30 zijazo watu hawatakubaliwa kutoka nje kati ya saa 21:00 na 06:00, alisema alipohutubia taifa.
"Huwa kwa kawaida napinga hali za tahadhari, lakini ilibidi niwalinde wananchi na kukomesha umwagikaji damu basi ikanabidi nifanye hivyo,” rais alisema.
Takriban watu 33 people walikufa mnamo wikiendi huko Port Said, ambapo uamuzi wa mahakama ulisababisha vurugu kuzuka.
Kutoridhika na uongozi wa Bwana Morsi's kulizua fujo kwingine nchini.
Katika mji mkuu wa Cairo, waadamanaji wailokuwa wanaipinga serikali walipambana na vikosi vya ulinzi karibu Uwanja wa Tahrir kwa siku ya nne mfululizo.

Upinzani

Upinzani unamlaumu Morsi kwa kutawala kimabavu na kuipa kipaumbele katiba mpya ambayo hailindi kikamilfu haki za kuabudu wala za maoni.
Serikali pia imelaumiwa kwa kutodhibiti hali ya uchumi, inayozidi kuzorota.
Aidha, aliwaalika viongozi wa kisiasa wakutane "katika majadiliano ya kitaifa " mnamo Jumatatu.
Ingawaje muungano mkubwa zaidi wa vyama pinzani nchini Misri, National Salvation Front, uliuunga mkono mualiko huo, ulilaumu sera za Morsi kwa kuzua vurugu.
Vurugu zilizuka Port Said baada ya mahakama kuwahukumu watu 21 kifo kwa kuhusika na fujo baada ya mechi ya kandanda Februari 2012.
Bwana Morsi alisema kwamba angechukua hatua zaidi "kwa ajili ya Misri" na kwamba ilikuwa "wajibu wake" kama rais kufanya hivyo.