Usiku wa jumamosi ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa bwana Mansour pale alipothibitisha kauli yake ya kuwa ipo siku atatimiza ndoto zake za kuitwa Mr Mansour,Harusi ya Mansour ilikuwa na matukio mengi ya kufurahisha na moja ya tukio zuri ni pale walipokuwa wakikata keki na mkewe...Pichani wakipata maelekezo toka kwa mtaalam kabla ya kuanza zoezi la ukataji wa keki hiyo.
Bi harusi ambaye ni mke wa bwana Mansour akionyesha kipande special cha keki ambacho alimlisha mumewe kwa staili ya aina yake...
''Pokea kiss special mke wangu na hii ni zawadi yangu kwako.''Maneno ya bwana harusi bwana Mansour kwa mkewe baada ya kulishwa keki...pembeni mwa maharusi ni wasaidizi maalumu wa maharusi wakishuhudia tukio la Kiss.
Pichani ni maharusi wakikata keki kwa ajili ya wageni waalikwa waliofika kwenye sherehe hiyo...Keki ilikuwa tamu na kila mmoja alipata sunna...Hongereni maharusi na mdumu milele kwenye ndoa yenu.


 Maharusi wetu walipendeza namna hii.....Hongereni tena jamani kwani mlipendeza..
Ndugu,jamaa na marafiki wa maharusi wakipata picha kama kumbukumbu