Na Richard Bukos MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo,
Irene Pancras Uwoya amezua jambo baada ya mume wa mtu, mkazi wa Kata ya
Kwadelo wilayani Kondoa, Dodoma ambaye jina lake halikupatikana,
kushindwa kuficha hisia zake za kimahaba na kuonesha waziwazi kumzimikia
staa huyo.Tukio hilo lilishuhudiwa na mwanahabari wetu hivi karibuni ambapo Uwoya
alikutana na mwanaume huyo kijijini Kwadelo alipokwenda na wasanii
wenzake, Jacob Steven ‘JB’ Wema Sepetu, Single Mtambalike ‘Richie’ na
Vincent Kigosi ‘Ray’ kuzindua mradi wa Kilimo Kwanza Ajira kwa Vijana
kwa mwaliko wa diwani wa kata hiyo, Omary Kariati. Baada ya kupata
nafasi ya kumuona Uwoya uso kwa uso katika maisha yake, mwanaume huyo
alifanya jitihada za hali ya juu kujipenyeza katikati ya wanakijiji
wenzake na kwenda kuweka pozi na staa huyo kisha kupiga naye picha huku
akimkagua kuanzia ukucha hadi unywele.Kama hiyo haitoshi, baada ya kugundua kuwa Uwoya ni mtu wa kawaida
tofauti na alivyomfikiria, alianza kumchezea nywele zake kimahaba huku
akitamani kuambatana naye kila alipokuwa akielekea kijijini hapo.
Kwa mujibu wa wanakijiji wenzake, jamaa huyo alikuwa akitamba kuwa
alimtaka Uwoya awe mkewe wa pili lakini aliishia kucheka tu bila
kumkubalia wala kumkatalia kwa kuwa alimchukulia kama shabiki wake wa
kawaida tu. Katika tukio hilo, mbali na kuzindua Kilimo Kwanza,
wasanii hao na Diwani Kariati, pia waliwakabidhi wanakijiji hao Sh. laki
tano zilizotolewa kama pole na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Mhe. Benard Membe kufuatia kijiji hicho kukumbwa na maafa ya
mafuriko hivi karibuni. |
0 Comments