Mwanajeshi wa Mali.
Kamanda wa majeshi ya Marekaini barani
Afrika, anasema kuwa makao makuu ya jeshi hilo, Pentagon ilifanya makosa
katika mafunzo iliyotoa kwa jeshi la Mali ambalo linakabiliwa na
kibarua cha kupambana na wapiganaji wa kiisilamu.
Generali Carter Ham wa kikosi cha jeshi la
Marekani Afrika, anasema kuwa majeshi hayo yalikosa kuwafunza wanajeshi
wa Mali kuhusu maadili ya jeshi.
Alikuwa akizungumza baada ya ripoti za mauaji ya raia yaliyofanywa na
jeshi la Mali wanaoshirikiana na wanjeshi wa Ufaransa kupambana na
wapiganaji hao.
Wakati huohuo, mashambulizi ya angani yameripotiwa Kaskazini mwa mji wa Gao.
Eneo hilo ambalo ni ngome ya wapiganaji hao,
ilianza kushambuliwa huku majeshi yakeindelea na harakati zao kwa wiki
ya tatu sasa. |
0 Comments