Wanataka kupewa haki sawa na watu wengine.

 Baraza la chini la bunge la Urusi, Duma, linatarajiwa kujadili muswada tata wa sheria ikilenga kuzuia inachokiita propaganda za mapenzi ya jinsia moja.
Kwa mujibu wa sheria mpya, matukio yote yanayohamasisha haki za wapenzi wa jinsia moja yatapigwa marufuku nchini kote Urusi, na waandaji wa shughuli hizo watatozwafaini

Wanaharakati wa ndoa za jinsia moja Urusi

Katika baadhi ya miji ya Urusi, ukiwemo St Petersburg, tayari wameanzisha sheria zinazopiga marufuku uhamasishaji wowote wa haki za wapenzi wa jinsia moja.
Wale wanaotetea muswada huo wanasema lengo ni kuwalinda watoto dhidi ya tabia hiyo. Hata hivyo watetezi wa haki za binadamu wamepinga sheria hiyo kwa kuiita kuwa ni hatari.

Wanaharakati wa ndoa za jinsia moja Urusi.Wakati huohuo, takriban wapenzi ishirini wa jinsia moja wametiwa nguvuni nje ya Majengo ya Bunge nchini Urusi wakijaribu kufanya maandamano ya kubusiana.Wanaharakati hao wanapinga hatua ya Bunge la Urusi la Duma, kutaka kupitisha Mswada unaopinga mapenzi ya jinsi moja na kupiga marufuku matukio yanayohimiza uhusiano kama huo kote nchini Urusi na waandalizi kutozwa faini.
Baadhi ya Miji ikiwemo St Petersburg, tayari imepiga marufuku matukio hayo. Wale wanaounga mkono Mswada huo wanasema ni muhimu kuwakinga watoto na maadili hayo yasiyofaa.