Na : Imelda Mtema
MKE wa aliyekuwa mcheza filamu
mahiri Bongo, marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Wastara Juma amesema
kuwa, gari na nyumba vitamuumiza maishani kwa kuwa ndivyo
vitakavyomkumbusha uwepo wa marehemu.
Akizungumza huku akilia kwenye
msiba wa mumewe nyumbani kwake, Tabata-Bima, Dar, Wastara alisema yeye
na Sajuki waliishi kama mapacha na kila walipokuwa wakitaka kutoka
walikuwa pamoja na mara nyingi marehemu ndiye aliyekuwa akipenda
kuendesha gari hilo kila walipokuwa wakienda.
0 Comments