Stori: Sifael Paul
AJUAYE uchungu wa mtoto ni mzazi!
Ukiwatazama akina mama watatu wa wasanii wa Tanzania waliofariki dunia
kwa nyakati na sababu tofauti hivi karibuni wakilia kwa uchungu, unaweza
ukadhani wazazi hao ni ndugu kwa namna nyuso zao zinavyoonekana kuwa na
majonzi mazito, Risasi Jumamosi linakuchambulia.Makabrasha ya gazeti hili yanawaonesha mama wa marehemu Steven Kanumba,
Flora Mtegoa, mama wa marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’, Zaina
Mkiety na mama wa marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Zaituni Mzena wakilia
kwa uchungu.
Wazazi hao walionekana wenye majonzi kupita maelezo
kwani kila mmoja alimbeba mwanaye tumboni kwa miezi tisa, akamlea,
akamtunza kwa tabu hadi akakua lakini baada ya kuanza kufaidi matunda
yao tu, Mungu akawachukua.
0 Comments