Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
IMEBAINIKA
kuwa lile gari la aliyekuwa nguli wa filamu Bongo, marehemu Steven
Kanumba, aina ya Toyota Lexus limekabidhiwa kwa mwigizaji, Mahsein
Awadhi ‘Dk. Cheni'Kwa mujibu wa chanzo makini, mama wa marehemu, Flora Mtegoa alifikia
uamuzi wa kumkabidhi Dk. Cheni gari hilo baada ya kushindwa kuligharamia
mafuta.
“Lilikuwa linakaa muda mrefu pale nyumbani kwao
Kimara-Temboni (Dar) bila kutumika ndipo bi mkubwa akaona bora amkabidhi
Dk. Cheni ili angalau aliendesheendeshe lisiharibike,” kilidai chanzo
hicho kwa sharti la kutochorwa jina lake gazetini.
DK. CHENI LIVE TABATA
Wakati mapaparazi wakianza
kazi ya kuchimba data zaidi juu ya gari hilo, Februari 9, walimnasa Dk.
Cheni akiingia na gari hilo kwenye arobaini ya marehemu Juma Kilowoko
‘Sajuki’ iliyofanyika nyumbani kwake Tabata-Bima, jijini Dar.
LIMEPIGWA BEI?
Kwa mujibu wa Dk. Cheni kwa sasa
gari hilo lipo mikononi mwake akilitumia kwa safari za hapa na pale ili
kulifanya lisiharibike vifaa kwa kukaa muda mrefu bila kutumika.
“Wamenipa nilitumie kwa muda kwani lingeendelea kukaa pale basi
lingeendelea kufa baadhi ya vifaa, wala halijapigwa bei,” alisema Dk.
Cheni.
Katika hatua nyingine, kauli ya mama Kanumba kuhusiana na
gari hilo ilitofautiana na ya mdogo wa marehemu, Seth Bosco ambapo mama
huyo alisema gari hilo halijatoka nyumbani huku mdogo mtu huyo akisema
limetoka.
“Mbona gari lipo hapa nyumbani halijatoka, kwanza limeisha bima na matairi hayana upepo sasa litatokaje?” alihoji mama Kanumba.
Seth alipoulizwa kuhusiana na uwepo wa gari hilo nyumbani, alitiririka:
“Gari limetoka kwa muda hata hivyo ni bovu na linahitaji marekebisho kidogo.”
0 Comments