Stori: Richard Bukos
BAADA ya mwanaye kutoka
mahabusu kwa dhamana, mama wa msanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael
‘Lulu’, Lucresia Karugila, hivi karibuni alinaswa akimpa mbinu mama wa
msanii Kajala Masanja zitakazomsaidia kumuokoa mwanaye.
Akina mama hao walinaswa na paparazi wetu kwenye Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo
Kajala na mumewe, Faraja Chambo walifikishwa kwa ajili ya kujitetea
kwenye kesi inayowakabili ya kutakatisha fedha haramu.Katika tukio hilo, mama Lulu ndiye aliyeanza kufika mahakamani hapo na
baada ya muda, alitokea mama Kajala ambapo walisimama chobingo na watu
waliokuwa karibu yao walidai mama Lulu alikuwa akimpa mwenzake mbinu za
kumwezesha kumuokoa mwanaye na kesi hiyo.
“Naona mama Lulu anampa
mwenzake mbinu za kumuokoa Kajala ila amefanya la maana sana kuja kumpa
kampani na kwa uzoefu wake wa mahakamani anaweza kumsaidia,” alidai mama
mmoja aliyekuwa karibu yao.Hata hivyo, wazazi hao walisitisha mazungumzo baada ya Kajala na mumewe
kutolewa chumba cha mahabusu na kupandishwa kizimbani ambapo Wakili wa
Serikali, Renald Swai aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 12 (kesho)
baada ya kupokea udhuru kutoka kwa hakimu aliyetakiwa kusikiliza kesi
hiyo, Sundi Fimbo.
Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, mama Lulu
aliendelea kuwa karibu na mama Kajala ila kilichowatawanyisha kilikuwa
ni mwanga wa kamera ya paparazi wetu.
0 Comments