Kundi la wake za watu walikuwa kwenye semina kuhusu namna ya kuishi kwa
upendo katika ndoa. Muwezeshaji akauliza, wangapi wanawapenda waume zao?
Wote wakanyoosha mikono. Akauliza tena, ‘Mara ya mwisho umemwambia
mumeo nakupenda lini?. Majibu mbalimbali yalitolewa, Wengine wakisema
Leo, wengine Jana, wengine hawakumbuki. Kisha akawaambia, kila mtu
achukue simu yake halafu amtumie mumewe text yenye maneno. NAKUPENDA
MPENZI, kisha wabadilishane simu. Wakaambiwa kila moja asome majibu
kwenye simu aliyoshika, majibu yalikuwa kama ifuatavyo;
Simu 1- Samahani nani mwenzangu?
Simu 2- He Mama Joji unaumwa?
Simu 3- Nami pia daima
Simu 4- Nini tena umeshagonga gari?
Simu 5- Sijakuelewa una maana gani
Simu 7- Umefanya nini tena? Leo sitakusamehe
Simu 8-Chukua taim yako
Simu 9-?!?
Simu 10- Acha kuzunguka unataka shilingi ngapi?
Simu 11 – Hivi naota?
Simu 12 – Kwa kweli leo usiponieleza hii mesej ulikuwa unampelekea nani atakufa mtu shenzi mkubwa
Simu 13 – Nilishakwambia usirudie kunywa pombe au ntakuacha naona umechoka kuishi na mimi
Tafadhali chukua dakika moja kumfahamisha mwenzi wako (mke/mume) kwamba unampenda ….
tahadhari: asije kuhisi simu imeibiwa!
0 Comments