MH! SIKU HIZI ANAJIFANYA SUPASTAA Akizungumza na
gazeti hili katika mahojiano maalum maeneo ya Magomeni, Dar, mganga huyo
alidai kuwa pamoja na jitihada kubwa alizofanya kumpaisha Diamond
lakini anamshangaa kwa kuwa amesahau alikotoka na anajifanya supastaa. Alidai kuwa siku hizi akimpigia simu, Diamond huwa hapokei, tofauti na zamani alipokuwa akihangaika kuchomoka kisanii. Mganga
huyo alifunguka kuwa sababu ya kufanya hivyo ni baada ya kuchukuliwa na
watu waliompeleka kwa waganga wa Kigoma ambako anajidanganya kuwa ndiyo
wanampaisha kumbe walimchukua akiwa ameshampandisha kwa kumpa dawa kali
za mvuto. ALIMPA DAWA GANI? Alizitaja dawa
alizompatia Diamond kuwa ni mitishamba aina ya Dubi, Ntajamasala (hii
humfanya watu wamuogope na kumheshimu), Italigula, Nkangacharo na Kalila
Lila (ambayo huichoma na kuoga kwa ajili ya kuwavutia watu). ANGUKO LA DIAMOND Alidai
kuwa Diamond amejisahau na hajui kama anguko lake linakuja kufuatia
ahadi aliyoiweka wakati anaanza kuimba baada ya kumpatia dawa hivyo
atapotea kwenye muziki. Akielezea historia ya kukutana kwao, Ustadhi
Yahya alisema yeye na staa huyo walikutana miaka ya 2000 nyumbani kwa
Papaa Misifa ambaye alikuwa meneja wa Diamond. Alidai kuwa kubadilika
kwa Diamond kulikuja baada ya kutwaa tuzo tatu za Kili mwaka 2010 ndipo
akawa anahusudu wanawake tofauti na masharti ya dawa japokuwa alimkanya
lakini hakumsikia.
DIAMOND ANASEMAJE? Kama
ilivyo desturi ya gazeti hili, lilimgeukia Diamond ili kupata mzani wa
habari hiyo ambapo alipopatikana kwa njia ya simu alisomewa maelezo yake
yote. AMKANA Katika maelezo yake, Diamond alikataa kata kata kuwa hamfahamu mtu huyo kisha akakata simu. “Sina msikiti nitakuwaje na Ustadhi? Huyo mganga nasema simfahamu,” alisema kisha akakata simu. |
0 Comments