Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia
.
HOJA binafsi ya mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia, imeibua mapya
bungeni mjini Dodoma, baada ya Kambi ya Upinzani kukutana kwa dharura,
kupinga kufifishwa hoja hiyo na Naibu Spika, Job Ndugai, wakidai anataka
kuizima.
Juzi Mbatia aliwasilisha bungeni Hoja Binafsi
kuhusu udhaifu wa elimu Tanzania, akitaka mfumo mzima unaosimamia elimu
nchini ufumuliwe. Baada ya majadiliano marefu kuhusu kuundwa kwa kamati ya kuchunguza mitalaa, sera na mihutasari ya elimu, hoja mbalimbali zilitolewa, baadhi ya wabunge wakitaka Kamati ya Bunge, huku wengine wakitaka iundwe tume huru ya kufuatilia suala hilo.
Mjadala huo uliendelea jana asubuhi kwa Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kusimama na kutetea
mfumo wa elimu uliopo na mtalaa, kabla ya wabunge kuchangia na Mbatia
kuhitimisha.
Akiwasilisha hoja yake, Mbatia aling’ang’ania
kupatiwa mtalaa wa masomo ya elimu kwa shule za msingi na sekondari,
jambo ambalo, Waziri Kawamba alijibu kuwa ulikuwapo ingawa hakuwa nao
bungeni.
Baada ya majibu ya Dk Kawambwa, Mbatia aliomba hoja yake iahirishwe hadi mtalaa utakapowasilishwa bungeni.
Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisimama na kusema akihoji:
“Katika kikao kilichopita, hata katika Hansard, tulisema mtalaa
utawasilishwa katika kikaohiki, sasa wasiwasi wa mbunge (Mbatia) ni nini? Hata siku ya mwisho ya Bunge tutaleta.”
Baada ya kauli hiyo, Naibu Spika, Job Ndugai
alipiga kura kwa kuuliza wanaotaka hoja imalizike na baada ya majibu,
aliruhusu Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangalla kuwasilisha Hoja Binafsi
kuhusu ajira kwa vijana na kilimo.
Hata hivyo, baada ya kumruhusu Dk Kigwangalla,
wabunge wa upinzani walitoka nje ya Bunge na kufanya mkutano wa dharura
uliochukua dakika 38 katika Ukumbi wa Pius Msekwa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti
wa kikao hicho, Tundu Lissu aliwaeleza sababu za wao kutoka nje ya
Bunge na hatua za kuchukua.
“Tumewaita kuzungumzia sababu za kutoka nje na
hatua za kuchukua. Kama mlivyosikia, Mbatia alisema kuwa hakuna mitalaa
wala hakujawahi kuwa na mitalaa tangu mwaka 1961 na kama ipo
atajiuzulu. Alipomtaka Waziri ampe japo nakala, waziri alikataa,”
alisema Lissu na kuongeza:
“Sasa tunachosema ni kwamba, Waziri Kawambwa
amelidanganya Bunge na tutapeleka taarifa ya kikao chetu katika Kamati
ya Bunge ya Mamlaka ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, kumtaka
ajiuzulu kwa kulidanganya Bunge, ikishindikana tutapeleka kwa Mamlaka
zilizomteua.” Alisisitiza: “Na hapa ikishindikana pia kumwajibisha, tutapiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.” Hata
hivyo, Lissu akiwa pamoja na Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema na Mbatia
meza kuu, alisema kuwa tangu kuanza kwa vikao vya Bunge, Spika Anne
Makinda na naibu wake Ndugai, wameonyesha nia ya kufifisha hoja za
upinzani.
Alisema: “Tulitaka kujadili hoja ya suala la
gesi ya Mtwara, lakini Spika akazima, akasema itaundwa tume, baadaye
akasema tume hakuna baada ya Waziri Mkuu kwenda, tangu Mbatia
kuwasilisha hoja yake, inaonekana waziwazi wanataka kuizima.”
Lissu aliongeza: “Kanuni ziko wazi, maspika
wamekula kiapo kufanya kazi bila upendeleo, lakini hapa hawatendi haki,
sasa sisi kama Kambi ya Upinzani, vilevile tutaandaa hoja kwa lengo la
kumwondoa spika na naibu wake.”
|
0 Comments