MSANII
wa muziki wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma 'Mwana Fa' aeleza, kuwa na
kipaji zaidi ya kimoja ndio sababu ya kipekee inayomtofautisha yeye
pamoja na kazi zake na baadhi ya wasanii wengine wa muziki wa bongofleva
Aliyazungumza
hayo jijini Dar es Salaam wakati akielezea mikakati yake aliyokuwa nayo
ya kuiachia nyimbo yake mpya hivi karibuni inayoitwa 'Kama
Zamani'ambapo mashabiki wake watapata fursa ya kuisikia nyimbo hiyo
katika vituo vya redio mbalimbali nchini, alisema kipaji ndicho
kinachompa fursa ya kufanya muziki katika ngazi ya kimataifa
Alisema
muziki unamatawi mbalimbali kwani kuna baadhi ya wasanii wanakipaji cha
kuimba tu lakini hawezi kufanya shoo katika 'stage' wapo baadhi wanajua
kuandika na hawajui kuimba wapo wengine wanajua kufanya vyote kwa
wakati mmoja
Akizungumzia kwa upande wake Mwana Fa alisema
amejaaliwa kuwa na vipaji vyote kwa wakati mmoja huku akiwa na uwezo wa
kuandika mashairi, kuimba pamoja na kulimiliki jukwaa pindi awapo katika
shoo
"Nimejaliwa vipaji vyote hivyo, kwani nina uwezo
wa kuandika mistari mizuri, kuimba na kulimiliki jukwaa na ndio maana
shoo zangu zinakuwa na mvuto wa kipekee kutokana, sanaa na ubunifu
niliokuwa nao " alisema Mwana Fa
Akizungumzia ujio wa wimbo wa
'Kama zamani' wenye mahadhi ya Hip Hop ambapo msanii huyo
amewashirikisha baadhi ya wasanii kama Man'dojo, Domokaya na The
Kilimanjaro Band (Wana Njenje), alisema kuwa ameamua kushirikisha
wasanii hao ili kuleta radha tofauti ya muziki na mashabiki
wapate muziki ulio bora
Alisema kuwa nyimbo hiyo italeta
mabadiliko makubwa katika tasnia ya muziki kulingana na ubora uliopo,
kwani imetengenezwa 'live' kinanda, gitaa vyote vinasikika kwenye muziki
huo, chini ya mtayarishaji Pfunk Majani
|
0 Comments