Watu wa tano leo asubuhi wamefariki dunia baada ya ndege ndogo waliokuwa wakisafiria kuanguka katika kiwanja cha ndege cha Charleroi nchini Hapa.Ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri toka Belgium kwenda France ilipata itilafu muda mchache toka iruke angani,Rubani wa ndege hiyo alijaribu kuirudisha ndege ardhini ila hali ilishindikana na ndege kuanguka na kusababisha vifo vya watu hao.
Watu walipoteza maisha ni watu wazima wawili na watoto wadogo watatu wa mwaka 2005,2006 na mwingiene wa mwaka 2010.Kiwanja cha ndege kilifungwa punde tu mara baada ya ajali kutokea...Inasemekana ndege ilikuwa na abiria watano ambao wote walifariki,kati ya abiria hao kulikuwa na mzee ambaye ni babu wa wajukuu watatu na mkwewe na wajukuu ambao wote kwa pamoja walifariki dunia.
Mamia ya wasafiri walikuwa uwanjani hapo kusubiri safari leo walishindwa kusafiri na baadhi ya ndege kushindwa kutua kiwanjani hapo kutokana na kufungwa kwa kiwanja hicho.Zaidi ya ndege 16 zilifanyiwa mabadiliko ya safari na zingine 5 kusitishwa kabisa kwa siku ya leo.Ndege zingine 15 zilichelewa kuanza safari kwa dakika 40 na zingine zaidi ya saa 6 kutokana na ajali hiyo.Charleroi Airport ni uwanja mdogo ambao ni maarufu nchini Ubelgiji upo kusini mwa Brussel.