SERIKALI ya Kenya inatafuta ufafanuzi kutoka kwa Serikali ya Marekani juu ya uhusiano baina yao mara baada ya uchaguzi mkuu kufanyika Machi 4. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkuu wa Utumishi wa Umma na Katibu wa Baraza la Mawaziri Francis Kimemia, alisema kuwa Serikali ya Kenya inamkaribisha kiongozi huyo kama alivyotoa tamko kwamba yupo tayari kufanya kazi na kiongozi yeyote ambaye watamchagua kama rais.
Kimemia alisema kuwa serikali inalazimika kutafuta ufafanuzi juu ya msimamo huo wa Marekani kama una ukweli baada ya Katibu Msaidizi wa wa masuala ya mahusiano Afrika, Johnnie Carson ambaye alitoa onyo kuwa chaguo la wakenya litasababisha madhara.
Hotuba hiyo iliyotolewa na Carson ilitafsiriwa na Serikali ya Kenya kama ni onyo na kwamba kutokana na uhusiano na nchi hiyo inawezekana wakapitisha Naibu Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza wake, William Ruto kuweza kuchaguliwa katika ofisi ya juu.
Viongozi hao Kenyatta na Ruto wanakabiliwa na makosa ya  uhalifu dhidi ya ubinadamu katika mashtaka Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC). Kimemia alisema kuwa hotuba ya Carson ilikwenda kinyume na ile ya  Rais Obama ambaye aliwahakikishia wakenya kuwa Serikali ya Marekani ilikuwa tayari kufanya kazi na mgombea yeyote ambaye Wakenya watamchagua.
Katika ujumbe aliotoa Rais Obama kwa njia ya video siku ya Jumanne, aliwahahakikishia wakenya kuwa Marekani haitoingilia mgombea yeyote ambaye atachaguliwa na wananchi wake katika uchaguzi huo mkuu.
Lakini kwa upande wake Carson, katika hotuba yake alisema kuwa uchaguzi ambao utafanyika utakuwa na madhara hali ambayo ilichukuliwa kama ni onyo na wananchi wa Kenya na kuwataka wananchi kuwa makini juu ya uchaguzi wao na hakumtaja Kenyatta wala Ruto katika hotuba hiyo.