Wadadisi wanasema kuwa serikali ya Rwanda huenda ikaghadhabishwa na hatua ya kuachiliwa kwa wawili hao.
Takriban watu 800,000, wengi wao wa kabila la Tutsi pamoja na waHutu waliuawa mwaka 1994, katika mauaji hayo ya kimbari.
Bwana Mugenzi alikuwa waziri wa biashara wakati
wa mauaji hayo wakati bwana Mugiraneza alikuwa waziri aliyehusika na
maswala ya wafanyakazi wa umma.
Mahakama maalum iliyoundwa kwa ajili ya mauaji
ya Kimbari Rwanda, (ICTR), iliwapata na hatia ya kuhudhuria mkutano
ambao uliamua kufurushwa kwa kiongozi wa eneo la Butare Kusini mwa
Rwanda, kwa kuzuia mauaji kufanyika.
Pia walipatikana na hatia ya kuhudhuria mkutano wa kaimu rais Theodore Sindikubwabo aliyewasihi watu kuwaua waTutsis.
'Mtu mwenye ushawishi'
Jaji wa mahakama ya rufaa, hata hivyo, aligundua
kuwa bwana Mugenzi na mwenzake Mugiraneza hawakujua kuwa nia ya
Sindikubwabo ilikuwa ni kutoa hotuba.
Majaji pia walisema kufurushwa kwa kiongozi wa
Butare, Jean-Baptiste Habyarimana, huenda ulikuwa uamuzi wa kisiasa na
wala sio kuharakisha mauaji ya kimbare.
Aidha wadadisi wamesema kuwa serikali huenda
ikakasirishwa sana hasa kwa kuachiliwa kwa bwana Mugiraneza ambaye
alikuwa mtu mashuhuri serikalini na aliyehusika pakubwa na mauaji ya
kimbari.
Serikali ya Rwanda inayoongozwa na waliokuwa
waasi wa KiTutsi na ambao walipigana dhidi ya serikali iliyosababisha
mauaji ya Kimbari, imekuwa ikikashifu vikali mahakama ya ICTR,na kusema
inajikokota pamoja na kugharimu pesa nyingi.
Lakini ICTR imekuwa ikijitetea ikisema kuwa kesi za Genocide katika mahakama za kimataifa huwa zina changamoto zake.
Mahakama ya ICTR inatarajiwa kufungwa mwaka 2014 baada ya kusikiliza kesi zingine 15 za rufaa.
Kulingana na mahakama hiyo, imesikiliza kesi 70
tangu kufunguliwa kwake kuambatana na azimio la baraza la usalama la
umoja wa mataifa Novemba mwaka 1994 hususan kusikiliza kesi za washukiwa
wakuu wa mauaji hayo. |
0 Comments