Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba. |
POLISI Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, linawashikilia watu kadhaa
kwa tuhuma za ujambazi walioufanya katika nyumba ya Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba Februari 3 mwaka
huu. Ujambazi huo ulifanywa wakati naibu waziri huyo akiwa safarini
jimboni kwake Bumbuli huku nyumbani hapo ikiwepo familia yake ambapo
mlinzi alifungwa kamba na kuzibwa mdomo na majamazi hao.
Katika tukio hilo majambazi hao hawakukamilisha
azima yao kwa kuwa mke wa naibu waziri huyo alibonyeza kengele ya
tahadhari mapema ambayo ilipiga kelele zilizowaogopesha majambazi hao
ambao walikimbia ili kujiokoa na kukamatwa. Baada ya tukio hilo,Kamanda
wa Polisi Kinondoni, Charles Kenyela aliahidi kuwasaka na kuwakamata
watu waliohusika.
0 Comments