Mgombea wa urais nchini Kenya Uhuru Kenyatta na
aliyekuwa mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura , wameitaka mahakama
ya ICC kuakhirisha kesi yake ili kuwaruhusu wajiandae.
Ombi hili limetolewa na mawakili wa Kenyatta na
Muthaura wakisema kuwa upande wa mashtaka ulichelewesha ushahidi wake na
hivyo hawakuwa na muda wa kutosha kujiandaa.
Mawakili wa wawili hao, Kari Khana na Stevenes Kay , walilalamika wakisema upande wa mashtaka unabadili mfumo wa kesi hizo.
Kenyatta, ambaye alikuwa waziri wa fedha
alishtakiwa kwa kuwa mmoja wa wahusika wakuu wa ghasia za baada ya
uchaguzi wa 2007/2008 ambapo zaidi ya watu 1,200 waliuawa na maelfu ya
wegine kuachwa bila makao.
Kufuatia ombi la mawakili hao la kuakhirishwa
kwa kesi hiyo,wadadisi wanasema huenda ikamfaa Uhuru hasa baada ya
uchaguzi mkuu tarahe nne mwezi Machi,
Wakiongea katika kikao mjini Hague, walisema
kuwa, kudumaa kwa shughuli za ICC , viongozi wa mashtaka waliwaacha na
ufahamu mdogo sana kuhusu kesi inayomkabili Uhuru na washukiwa wenzake.
"tunataka mashtaka haya kuchunguzwa vyema, ''
alisema wakili wa Uhuru, Steven Kay, ambaye alisema hata hajapata muda
wa kupitia ushahidi uliotolewa.
Kenyatta, ambaye alifuatilia kikao hicho kwa
video akiwa nchini Kenya, alisema mara moja tu kuwa alielewa bado
anaweza kutakiwa kufika Hague na majaji wa kesi hiyo.
Wawili hao pamoja na washukiwa wengine watatu,
akiwemo mgombea mwenza wa Uhuru , william Ruto wanakabiliwa na kosa la
kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi.
Mawakili hao pia walikosoa upande wa mashtaka na kusema kuwa walikubali kutumia mashahidi waliotoa ushahidi wa uongo. |
0 Comments