Jumuiya ya Nchi za Ulaya inaziomba nchi wanachama kuchunguza nyama mara kwa mara.
Nchi hizo zimeombwa kufanya hivyo ili kudhibiti kashfa inayozidi kuenea kwa kasi kuhusu nyama ghushi ya farasi.
Kwa muda wa miezi mitatu kutokea Machi 1, wanachama wote watatakiwa kuzifanya uchunguzi wa DNA nyama za ng’ombe zinazoongezwa kemikali za kuzihifadhi, ili kuona kama zina dalili zozote za nyama ya farasi, alisema mwenyekamati anayesimamia maswala afya barani Ulaya Tonio Borg.
Alikuwa akiongea mjini Brussels baada ya mkutano na mawaziri kutoka Uingereza, Ufaransa, na nchi nyingine zilizouziwa nyama ya farasi.
Hatua

Hatua hizi zilifuatia ugunduzi kwamba nyama iliyokuwa imeuziwa takriban nchi 16 za Ulaya kama kuwa ni ng'ombe, ilikuwa imejumuishwa na ya farasi.
"Mtu fulani katika biashara ya chakula aliamua kuuza nyama ya farasi kama ya ng’ombe, na hivyo kuchuma pesa kilaghai," alisema Simon Coveney, waziri wa kilimo wa Ireland.
Kutuliza umma
Kwa sasa kuna haja kubwa ya kuituliza umma, lakini tatizo ni kwamba jumuiya hiyo na mawaziri wake hawana majibu kwa maswali yote.
Waziri Mkuu wa Romania Victor Ponta amesema kwamba kashfa hiyo ilikuwa 'ya utapeli na ulaghai wa hali ua juu'.
Sasa watu wanatoa wito kwamba nyama zitakazouziwa jumuiya hiyo ya Ulaya zinafaa zionyeshe wazi zitokako. Lakini kufanya hivyo kunaweza kukazua malalamishi kutoka kwa wenye viwanda vya chakula kwa sababu ya uwezekano wa kuongezeka kwa gharama.