Mugabe na Tsvangirai |
Zimbabwe inapigia kura ya maoni kielelezo cha katiba
hii leo, ikiwa ni mara ya kwanza tangu uchaguzi ufanyike nchini humo
uliokumbwa na utata mwaka wa 2008.
Hata hivyo malalamiko yametolewa kuwa huenda
nchi hio haijajiandaa vilivyo kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha na
wachunguzi wanadai kuwa wamefungiwa nje ya shughuli hiyo.wapiga kura katika foleni |
Katiba hiyo inapendekeza kuhifadhiwa nafasi ya rais mwenye nguvu nyingi serikalini na hii inampa rais Mugabe uwezo wa kusalia madarakani kwa miaka kumi zaidi.
Hata hivyo kura hii ya maoni haijawachangamsha sana wananchi wa Zimbabwe huku raia wengi wakionekana kulenga zaidi uchagzui mkuu unaopangwa kufayika miezi chache zijazo.Katiba mpya inatazamiwa kunyoosha njia ya kufanyika uchaguzi huo mkuu japo kuna wasiwasi kwa machafuko zaidi kutokea nchini humo.
0 Comments