Maofisa watano wa Jeshi la Polisi nchini wamefikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na
shtaka la wizi wa Sh150 milioni. Akiwasomea hati ya mashtaka
yanayowakabili, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benard Kongora aliwataja
washtakiwa hao kuwa ni sajenti Dancan Mwasabila (43) Koplo Geofrey
(39).
Wengine ni Koplo Rajabu Nkumkwa (46), Koplo
Kawanani Hamphrey (34) pamoja na Koplo Kelvin Mohamed (44). Kongora
alidai kuwa Desemba 18, 2012 katika eneo la Kariakoo Wilaya ya Ilala,
washtakiwa hao kwa pamoja waliiba fedha taslimu Sh150 milioni mali ya
Mire Artan Ismail.
Washtakiwa wote walikana shtaka hilo na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.Hakimu Mchauru aliwataka washtakiwa hao kila mmoja kusaini bondi ya Sh5
milioni na kuwasilisha fedha taslimu Sh15 milioni ama hati ya mali
isiyohamishika yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha. Mbali na masharti
hayo ya dhamana, pia kila mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili
wanaoaminika ambao kila mmoja wao angesaini bondi ya Sh5 milioni. Kesi
hiyo itatajwa mahakamani hapo Machi 27.
0 Comments