Dar es Salaam.
 Hospitali ya Kairuki ya Mikocheni inatarajiwa kwa mara ya kwanza kutoa huduma ya kuzalisha wanawake kwa njia ya chupa mara ujenzi wa jengo lao la kisasa utakapomalizika.
Teknolojia hiyo ya kisasa na pekee kwa aina yake, itaifanya hospitali hiyo kuwa ya kwanza binafsi Tanzania kuzalisha wanawake kwa njia ya chupa,’In vitro fertilisation (IVF)’.
Mkurugenzi Msaidizi wa Hospitali ya Kairuki, Clementina Kairuki, alisema jana kuwa jengo hilo la ghorofa sita linatarajiwa kujengwa Mikocheni, jirani na eneo ilipo hospitali hiyo.

Kairuki ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kwenye hospitali hiyo, alisema tayari mkakati wa awali wa ujenzi wa jengo hilo  umeanza.
Akifafanua alisema ujenzi wa jengo hilo unatarajia kutumia  Sh7.2 bilioni na kwamba, mbali na huduma ya IVF pia litakuwa linatoa huduma kwa watoto.
“Dhamira ya hospitali yetu katika ujenzi wa jengo hili, ni kuhakikisha uzazi salama kwa wanawake wajawazito Tanzania na kuunga mkono jitihada malengo ya Milenia kimataifa na kitaifa,” alisema Kairuki.
Kuhusu jengo hilo, alisema sehemu ya juu kutakuwa na uwanja wa ndege (helikopta), ghorofa moja itakuwa kwa ajili ya maegesho ya magari madogo yasiyopungua 32.
Aidha, kutakuwa na vyumba vya mionzi  vyumba vya wagonjwa mahututi,
eneo la matibabu ya dharura, wodi za kulala