Shughuli ya kuhesabu kura
Siku nne baada ya kupiga kura wakenya wangali kujua mshindi, wa urais, baadhi ya yaliyojitokeza hadi sasa ni pamoja na malalamishi ya muungano wa CORD wake Raila Odinga kutaka tume ya uchaguzi kusitisha shughuli ya kuhesabu kura wakidai kufanyika udanganyifu.
Leo mashirika ya kijamii yamekwenda mahakamani kuitaka mahakama kuu kusitisha shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura
Nayo tume ya uchaguzi yasema idadi kubwa ya kura zilizoharibika ilitokana na hitilafu katika mtambo wake ambao ulikuwa unaongeza idadi ya kura hizo mara nane
Matokeo hadi kufikia sasa Raila Odinga ana kura 4,516,660 wakati Uhuru Kenyatta ana kura 5,159,344
Wakenya wakiwa katika kipindi kigumu na cha wasiwasi kwani imechukua Tume ya Uchaguzi muda wa siku nne tangu kuanza shughuli ya kuhesabu kura na bado mshindi hajajulikana.

Kumekuwa na kila aina ya matukio katika muda huo wote. Tayari mashirika ya kijamii yameitaka mahakama kusitisha shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura inayofanywa na tume ya uchaguzi.Muungano wa CORD unaoongozwa na tume ya uchaguzi, umelalamika ukisema shughuli hiyo ina mizengwe na wanataka ianzishwe upya.
Tupe maoni yako kwenye ukurasa wetu wa Bofya Facebook kuhusu yanayojiri Kenya na tutauweka ujumbe wako kwenye mtandao wetu Bofya bbcswahili.com
18:26 Mwandishi wa BBC Idriss Shituma abaye yuko katika ukumbi wa Bomas, anasema kuwa hadi sasa kura zilizoharibika zimefika 93, 385 wakati shughuli ya kuhesabu kura za urais ikiwa bado inaendelea katika ukumbi huo
17:56 Vincent Koe Kutoka Kericho Kenya anasema kupitia Bofya facebook kuwa subira anayo lakini hali hii kuchelewesha matokeo inawavunja moyo watu wengi na kuwaumiza matumbo
17:50 Matokeo hadi kufikia sasa Raila Odinga ana kura 4,516,660 wakati Uhuru Kenyatta ana kura 5,159,344
17:49 Mahakama kuu nchini Kenya imetupilia mbali kesi iliyokuwa imewasilishwa na mashirika ya kijamii dhidi ya tume ya uchaguzi wakiitaka isitishe shughuli ya kuhesabu kura za urais. Walidai kuwa tume hiyo inahujumu matokeo hayo.Mahakama imeyataka mashirika hayo kuiwasilisha kesi hiyo katika mahakama ya juu zaidi
17:30 Hadi kufikia sasa Uhuru Kenyatta ana kura 5,159, 344 na Raila Odinga amepata 4,516,660 baada ya kura 10,339,978, kuhesabiwa.
16:45 Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Ahmed Isaack Hassan amewaambia maajenti wote wa vyama vya kisiasa ambao wana tashwishi kuhusu shughuli ya kuhesabu kura za urais waweze kuwasilisha malalamishi yao kwa tume ya uchaguzi baada ya shughuli hiyo kukamilika .Wameelezea kuwa shughuli hiyo inafanywa kwa njia ya uwazi na ambayo iko wazi kukaguliwa na mtu yeyote 42534
16:41 Oswago amesema alipokea ujumbe wa simu uliosema kuwa kesi iliyowasilishwa na mashirika ya kijamii kutaka mahakama kusitisha shughuli ya tume ya uchaguzi kujumlisha matokeo ya kura za urais, imepuuziliwa mbali na mahakama
16:34 Bwana Oswago pia amesema kuwa hayuko jela wala hajafariki kwani kulikuwa na tetesi kuhusu hali yake mapema leo.Ameelezea kuwa shughuli hii ya kujumlisha matokeo ya kura za urais lazima ikamilike leo
16:31 Afisaa mkuu mtendaji wa tume ya uchaguzi nchini Kenya James Oswago amehutubia wakenya kuwaeleza kuhusu njia ambayo tume ya uchaguzi imetumia kujumlisha matokeo ya uchaguzi wa Urais ambayo hadi kufikia sasa yanaonyesha Uhuru Kenyatta kuwa mbele ya mpinzani wake Raila Odinga
16:10 Mwandisi wa BBC Ann Mawathe ambaye yuko mjini Kisumu ngome ya Raila Odinga anasema kuna hali ya utulivu watu wameanza kurejea kazini na ingawa bei ya bidhaa imeanza kuwa ghali kutokana na wafanyabiashara kuwa na hofu kwenda maeneo jirani kununua vyakula hadi matokeo yatakapotangazwa.
15:55 Hadi sasa Uhuru Kenyatta ana kura 5,115,704 huku Raila Odinga akiwa na kura 4,513,223. Zaidi ya kura milioni kumi zimehesabiwa huku matokeo yakitarajiwa kutoka maeneo bunge mangine chini ya thelathini
15:49Nyora Wahome kwenye ukurasa wa Bofya facebook anasema amechoka kusubiri kwani amengoja saana
15:40Dennis Tsunami Mbaka anasema kupitia Bofya facebook mataraiio ya wakenya ni mengi na licha ya kuzuka mambo mengi wakati huu wa uchaguzi hususan matokeo ya uchaguzi wa urais yakisubiriwa, anachotaka ni mchakato mzima kukamilika bila tashwishi na anaitakia nchi yake mustakabali mwema
15:32 Kuhusu kesi ambayo mashirika ya kijamii yameishtaki tume ya uchaguzi na kuitaka ikomeshe shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura za urais, ni mapema mno kwa hilo. Duru za kisheria zinasema kuwa kesi hiyo ina misingi duni kwani wanapaswa kusubiri matokeo rasmi ya uchaguzi kutangazwa ndiposa waende mahakamani
15:25 Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Isaack Hassan anatarajiwa kuhutubia waandishi wa habari wakati wowote kuanzia sasa
15:21Hanif Mohammed akiwa mjini Mombasa ameandika kwenye ukurasa Bofya facebook akizungumzia matokeo ya uchaguzi kwa sasa ya wagombea wakuu kuwa wanakanganywa na hesabu ya kura hizi ila anachoomba tu ni kuwepo amani
15:14 Sebastian Sabato kwenye ukurasa wa Bofya facebook anasema, ijapokuwa ninasubiri matokeo kwa hamu na gamu, kwa upande mwingine shughuli zangu zinaendelea kama kawaida.