Tarehe 23/3/2013 ilikuwa siku ya kuzaliwa kwa Tyrisha...Pichani Tyrisha akijiandaa kuzimisha mishumaa na kukata keki.
Hawa ndio wazazi wa Tyrisha  wakijiandaa kulishwa keki na binti yao ambaye haonekani pichani.
Muziki special ulifunguliwa rasmi na wazazi wa Tyrisha kama mnavyojionea pichani.
Ulipofika muda wa Tyrisha kukata keki kila mmoja alimsapoti kwa kumpigia makofi ya furaha 
Na muda wa chakula ulipoiwadia kila mgeni alipatiwa alichotaka kwa siku hiyo.
Bibi wa Tyrisha akiinuka kwa furaha na mkwewe tayari kwa kucheza muziki na mjukuu wao.
Huyu ni mama mdogo wa Tyrisha 
 Dada zangu pia walikuwepo
Dj wa kijiji ambaye ukonga nyoyo za wageni pindi akifanya makamuzi yake kama mnavyomuona.
Muheshimiwa mstahiki Meya wa Sluis bwana Mohammed akishiriki katika kulisakata rumba na mkewe kipenzi.
Katika wageni waalikwa waliohudhuria sherehe ya Tyrisha bidada Fatma Mashauzi Classic pia nae alikuwepo.Pichani akiwa na New Baby born bidada Nuhrat ambaye siku chache zijazo tunatarajia sherehe babu kubwa  ambayo wengi wao wanaisubiri kwa hamu.