Na. Mwandishi Wetu
MPIGAPICHA wa kujitegemea ambaye ni mlemavu wa miguu wa mjini hapa, Elias Ngole Ngoswe amemwangukia msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu kwa kumuomba msaada ili aweze kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wetu Jumanne iliyopita, Ngoswe ambaye ulemavu wake ulitokana na kugongwa na gari kwenye mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe, Februari 2, mwaka jana na akavunjika miguu na mfupa wa nyonga, alisema uamuzi wake wa kumuomba msaada Wema unatokana na kuvutiwa kwake na msaada aliompa msanii mwenzake, Kajala Masanja ambaye alimuokoa kufungwa jela kwa kumtolea faini.
“Nimegundua kuwa Wema ana huruma sana nami nikaamua nimuombe msaada kupitia gazeti hili kwani nina matatizo mazito. Nilipovunjika miguu na nyonga nilikimbizwa Hospitali ya Wilaya Magunga, Korogwe baadaye nikahamishiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha, nikalazwa miezi mitatu baadaye nilihamishiwa Muhimbili ambako bei niliyoandikiwa nilipe imenishinda,” alisema Ngoswe.
Kwa mujibu wa hati ya malipo ya Muhimbili ya Septemba 10 mwaka jana (nakala tunayo), Ngoswe alitakiwa alipe gharama za matibabu shilingi 9,798,250 ambazo hana.
“Ni fedha nyingi sana ambazo kutokana na ugumu wa maisha, nimeshindwa kulipia. Namuomba Wema na watu wengine wenye huruma wanisaidie ili nitibiwe,” alisema kwa masikitiko Ngoswe. Wema au yeyote aliyeguswa na habari hii awasiliane naye kwa namba 0766 224 284 na Mungu atawabari