Stori: Issakwisa Mponi Na Denis Mtima
Huku vuguvugu la Uchaguzi Mkuu 2015 likianza kwa kasi, gazeti hili kwa kushirikiana na jeshi la polisi nchini wamefanikiwa.kunasa vitambulisho feki vya kupigia kura.
Vitambulisho hivyo ambavyo kwa muonekano havina tofauti na vile ‘orijino’ vinavyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi vilinaswa ndani ya ‘steshenari’ moja inayomilikiwa na mwanamke aitwaye Levina Mapunda iliyopo Tabata Mawenzi jijini Dar.
MCHEZO ULIVYOANZA
Hivi karibuni mmoja wa raia wema alipiga simu katika chumba chetu cha habari na mahojiano yalikuwa hivi;
Raia mwema: Hapo ni Global?
Mhariri: Hujakosea, tukusaidie nini?
Raia mwema: Nyie si mnasema mnafichua maovu? Njooni huku Tabata kuna mtu anafoji vitambulisho feki vya kupigia kura.
Mhariri: Kibali cha kufanya hivyo kapewa na nani?
Raia mwema: Mimi sijui, nyie njooni mshuhudie.
GLOBAL YATINGA POLISI
Kufuatia taarifa hizo, waandishi wetu walikwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi Buguruni ambapo walipewa maafande na
kuongozana nao hadi eneo la tukio.
WAANDISHI, ASKARI WAVAMIA ‘STESHENARI’
Katika kufanikisha zoezi la kumnasa mtu huyo, polisi walimtanguliza askari mmoja wa kike ambaye alifanya upelelezi wake wa awali na wakati akiwa mle ndani, aliingia kijana mmoja na kutaka apewe kitambulisho chake feki cha kupigia kura alichotengenezewa.

MTEGO WANASA
Baada ya kijana huyo kukabidhiwa kitambulisho hicho, yule polisi wa kike aliwapa ‘signo’ wenzake waliokuwa nje ambao walivamia

na kumtia nguvuni Levina.
Baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo, polisi hao walifanya upekuzi wakiwa na mjumbe wa serikali ya mtaa wa eneo hilo na kufanikiwa kupata nyaraka nyingine feki kama vile vyeti mbalimbali vya kuhitimu elimu ya sekondari, vyeti vya kuzaliwa, leseni

za udereva, vyeti vya kuhitimu vyuo na vitambulisho feki vya kazi na shule.
Levina alichukuliwa hadi polisi pamoja na kompyuta yake iliyohisiwa kuwa na nyaraka nyingine.