Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na waziri mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Nicolas Tiangaye, wamekutana mji mkuu wa Afrika Kusini, Pretoria, na wamekubaliana kuzidisha uhusiano baina ya nchi mbili hizo.Uhusiano uliharibika baada ya wanajeshi 13 wa Afrika Kusini kuuwawa mwezi March wakati wapiganaji walipoiteka serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Vyombo vya habari vya Afrika Kusini viliarifu kuwa wanajeshi hao walipelekwa huko ili kampuni za biashara za Afrika Kusini zipate kandarasi za madini nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Wakuu wa Afrika Kusini walikanusha hayo