Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete (Watatu kulia), Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Gaudentia Kabaka (Wanne Kulia), Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya (Wakwanza kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Profesa Adolf Mkenda (Wapili Kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick (Wapili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (Wakwanza kulia), wakiimba wimbo wa taifa mwanzoni mwa sherehe za miaka 10 ya fao la elimu litolewalo na Mfuko huo. Sherehe hiyo ilifanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya fao la elimu la Mfuko wa Pensheni wa PPF, kwenye sherehe iliyofanyika juzi kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio na Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Angellah Kairuki.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akipokea zawadi toka kwa naibu waziri wa fedha, Saada Mkuya Salum kwa niaba ya PPF kwenye sherehe za miaka 10 ya Fao la Elimu litolewalo na Mfuko huo kwa watoto ambao wazazi wao walikuwa wanachama wa Mfuko huo kabla ya kufariki. Sherehe hizo zilifanyika Jumamosi iliyopita kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.