Mrs Beyoncé Carter
Kwa mara ya kwanza katika historia yake ya muziki bidada Beyoncé hivi majuzi nchini Belgium alihairisha show yake kwa kutojihisi vizuri kiafya.Beyonce aliyekuwa akisubiriwa na wengi katika show aliyotarajiwa kuifanya siku ya jumanne katika mji wa Antwerpen nchini Ubelgiji ilibidi awaombe radhi wapenzi wake wote waliokuwa wamejiandaa kwa siku hiyo ila alifanya show siku iliyofuata yani jumatano.Kwa harakaharaka Beyoncé aliutangazia umma kwamba ameombwa na daktari kupata mapumziko ya kutosha kutokana na uchovu alionao...ila habari ambazo zinazagaa kwa sasa kila kona ya dunia ni kwamba hali hiyo iliyomfanya Beyoncé kujihisi vibaya inasababishwa na Ujauzito aliona hivi sasa.Kama kweli basi Beyoncé anatarajia kupa mtoto mwingine hivi karibuni.