Young Africans ambayo imetwaa ubingwa baada ya kufikisha pointi 57 itashuka dimba la uwanja wa Taifa kuhakikisha inaendeleza wimbi la ushindi katika michezo yake kwani tangu kuanza kwa mzunguko wa pili Yanga haijapoteza mchezzo hata mmoja.
Kocha Mkuu Ernie Brandts amesema kikosi chake kipo fit, kiakili, kifikra, kiafya na morali ya wachezaji ni ya hali ya juu hivyo wana kila sababu ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo kwakua Yanga kwa sasa ina kikosi bora kuliko timu zote katika ukanda wa Afrika Mashariki.

                                                Watani wa jadi leo ndio leo.....