“Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo watoto wana lishe duni zaidi. Kwa mfano, takwimu zinasema kuwa asilimia 42 ya watoto wote wana lishe duni,” alisema na kuongeza kuwa lishe duni inasababisha watoto wasiwe werevu darasani na kuwa na malezi duni.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Roswita Kasikila alielezea kukerwa kwake na deni la Sh52 bilioni ambalo Bohari ya Dawa (MSD) inaidai Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akisema linaifanya bohari hiyo kuwa dhaifu kiutendaji.
“MSD inafanya kazi kama mama lishe, mpaka iuze dawa ndipo inunue dawa nyingine? Ndiyo maana inashindwa kufanya kazi vizuri,” alisema Kasikila.
Aliitaka Serikali kulipa deni hilo ili MSD inunue dawa na vifaa tiba vya kutosha kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya nchini.
Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Magdalena Sakaya alimtuhumu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Kombe, Kata ya Usinde, Tabora akisema ana tabia ya kulewa akiwa kazini na kuwauzia wajawazito kadi za kliniki.
Sakaya alisema daktari huyo baada ya kushtakiwa kwa tabia zake za kuuza kadi za kliniki na kulewa akiwa kazini, aliwalipizia kisasi waliomshtaki kwa kukataa kuwatibu.“Alikataa kumtibu mke wa mtu aliyemshtaki ambaye alikuwa mjamzito. Hata mtoto alipozaliwa aligoma kumpa chanjo na matokeo yake mtoto alipoteza maisha,” alisema.
Aliitaka Serikali kumfukuza kazi daktari huyo badala ya kumhamishia wilaya nyingine.
0 Comments