Kuna hofu kuwa huenda maandamano kama yaliyoshuhudiwa mwaka
jana yakatokea
Kampuni ya uchimbaji madini ya Lonmin, nchini Afrika Kusini inasema kuwa maelfu
ya wafanyakazi katika mgodi wake wa wa platinum wamefanya mgomo kinyume cha
sheria baada ya afisa wa muungano wao kupigwa risasi katika baa moja mwishioni
mwa juma.Msemaji wa kampuni hiyo Sue Vey amesema kuwa shughuli zote za uzalishaji kwenye
kiwanda hicho zimevurugika .
Mgomo huu umezua hofu ya vurugu zaidi kutokea baada ya sekta hiyo kukumbwa na
migomo mwaka jana
Mwezi Agosti mwaka jana wafanyakazi thelathini na wanne waliuliwa na polisi
katika mgodi wa Marikana na waandishi wa habari wanasema mgomo huo umesababisha
hofu ya kutokea kwa ghasia kufuatia hali ya taharuki iliyopo juu ya kukatwa kwa
kazi , mashauriano ya riba na uhasama ndani ya muungano wa wafanyakazi.
Lonmin, ambayo hisa zake,ziko katika soko la hisa la London na Johannesburg ,
ndiyo kampuni ya tatu kwa ukubwa katika kuzalisha madini ya platinum.
Taarifa za mgomo wa leo zimesababisha hisa za kampuni hiyo kushuka kwa
asilimia 5% mjini London.
Msemaji wa kampuni hiyo, Sue Vey alisema kuwa migodi yote kumi na mitatu ya
kampuni hiyo imefungwa kwa sasa.
"Wafanyakazi wa kampuni hiyo waliwasili kazini ingawa hawakuelekea katika
shughuli zao kama ilivyo desturi yao
Huku akisema kuwa kampuni hiyo haielewi kwa nini wafanyakazi wameamua kugoma,
msemaji wa chama cha wafanyakazi hao, alisema kuwa huenda mgomo huo unatokana na
ghadhabu ya wafanyakazi hao, kuhusu mauaji yaliyotokea mwishoni mwa wiki ya
kiongozi mmoja wa chama hasimu cha wafanyakazi.
Polisi walithibitisha kuwa kiongozi huyo aliuawa mwishini mwa wiki katika
eneo Rustenburg. |
0 Comments