“Najisikia vibaya huyu ni mdogo wangu, lakini bomu limemfanya apoteze furaha yake, tazama anavyotapika kila anachokula, lakini tutaendelea kumtazama Mungu,” alisema Malamsha ambaye naye ni mkazi wa Olasiti.
Kijana huyo ni miongoni mwa majeruhi saba waliofikishwa MNH kwa matibabu zaidi, baada ya kujeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu uliotokea katika Kanisa Katoliki la Mtakafitu Joseph Mfanyakazi.
Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa MNH, Jeza Waziri alieleza kuwa majeruhi karibu wote wanaendelea vyema,baadhi yao wanaweza kuruhusiwa kurejea nyumbani kwao hasa kutokana na hali zao kuendelea kuimarika.
Majeruhi wengine ni Gabriel Godfery (9), Jenipher Joachim (40) na Anastazia Regnard (14).
Wengine ni Albert Njau (35), Faustine Shirima (33) Fatuma Tarimo (38) ambaye amepimwa na kuonekana ana chembechembe za vyuma vya bomu ndani ya tumbo lake.
0 Comments