Na Abdulaziz video/Lindi yetu Blog

Redd’s Miss Lindi 2013 atajulikana Usiku wa tarehe 31 may,2013 ndani
ya ukumbi wa Lindi Beach Resort. Jumla ya Warembo Kumi watachuana
Vikali kugombania taji hilo. 
 

Warembo hao wako kambini Hotelini hapo
kwa mazoezi makali huku wakiongozwa na Redd’s Miss Lindi 2012. 

Mratibu wa Mashindano hayo Ndugu Justine alisema Mwaka huu wamejiandaa
vizuri na warembo wako katika hali nzuri ya kiafya kambini hapo na Pia
anataraji show itakuwa ya Kihistoria kwa jinsi maandalizi yalivyo
andaliwa, hivyo amewataka wadau kujitokeza kwa wingi. 

 Viingilio vimetajwa kuwa viti vya kawaida siku hiyo vitakuwa Tsh
10,000/= na VIP itakuwa 15,000/= na tiketi zitaanza kuuzwa siku hiyo
hiyo ya tarehe 31/05/2013 majira ya asubuhi Hivyo wahi tiketi yako
mapema ili ushuhudie show ya kihistoria katika mambo ya urembo katika
mji wa Lindi.