Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa nne kushoto)akiwa na ujumbe wake katika mazungumzo na Rais wa China Xi Jinping,(wane kulia) katika Ikulu ya Mjini Beijing Nchini China leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Makamo wa Rais wa China Li Yuanchao,katika makaazi yake Mjini Beijing nchini China akiwa katika ziara ya mualiko wa Kiserikali wa Nchi hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwatambulisha Viongozi katika ujumbe aliofuatana nao kwa Rais wa Jamhuri ya watu wa China Xi jinping, walipofika Ikulu ya Mjini Beijing Nchini China akiwa katika ziara ya mualiko wa Serikali wa Jamhuri hiyo.